Monday, November 15, 2010

Vichaa wacha tu.... 


Kichaa mmoja alikua yuko wodini juu ya baiskeli aliyopewa na dokta wake. Baiskeli ikawa imewekwa kwenye stendi, kwa hiyo akawa anaendesha iko palepale. Dokta akawa anamuangalia anaendesha kwa kasi mno baada ya mda akatulia. Dokta kuona kichaa amekaa mda mrefu juu ya baiskeli bila kufanya lolote, akamfata akamuuliza.

"Vipi mbona huendeshi baiskeli?"

kichaa: Shhhh, niko kwenye mteremko.

Dokta huyo akaondoka.

No comments: