Wednesday, December 01, 2010

Leo ni siku ya UKIMWI

duniani


Virusi Vya UKIMWI (VVU) husababisha UKIMWI (Upungufu waKInga MWIlini) ambao sasa ni tatizo la dunia. Mwaka 2009 Shirika la Afya Duniani (WHO) ilikadiriwa kuwa watu milioni 33.3 wana virusi vya VVU


UKIMWI HUSABABISHWA NA NINI?

Ukimwi husababishwa na VVU. VVU hushambulia kinga ya mwili na kuusababisha ushindwe kupigana na magonjwa. Inaweza kuchukua miaka mingi kwa dalili za ugonjwa kujionyesha tokea unapoambukizwa. Hivyo mtu akionekana ya kwamba ana siha nzuri, siyo kwamba mtu huyu hajambukizwa VVU.

VVU hupatikana katika damu, shahawa na majimaji katika uke. Uambukizaji hutokea wakati VVU inapotokea katika mwili wa mtu aliyeambukizwa na kuingia katika mzunguko wa damu wa mtu mwingine.


Hii hutokea kwa jinsi zifuatazo:

Kujamiiana bila ya kutumia kondomu kwa njia ya uke, njia ya haja kubwa (kulawitiana) na  kutumia midomo.

Ngozi kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali kilicho na virusi vya ukimwi kama nyembe za kunyolea na kutahiria na sindano zinazotumika kuchorea miili, kutogea masiko, kuchanjia na kwa ajili ya huduma za afya katika nchi zinazoendelea. Mgonjwa kupewa damu iliyoambukizwa na VVU.


HUWEZI KUAMBUKIZWA KWA NJIA ZIFUATAZO
Mbu, kusalimiana, makalio ya vyoo vya kukalia, kukohoa au kupiga chafya, kuogelea.


JINSI YA KUJIZUIA NA KIRUSI CHA ( HIV)

Kuacha kujamiiana ndiyo njia pekee ya kujizuia na magonjwa ya zinaa na ni vigumu kwa kweli, hivyo basi wakati wa kufanya mapenzi tumia kondomu kwa usahihi. Kondomu inayotumiwa kwa usahihi ndiyo njia pekee ya kujizuia dhidi VVU na magonjwa mengine ya zinaa. Dawa za uzazi wa majira haziwezi kuzuia maambukizo ya UKIMWI


No comments: