Tuesday, December 28, 2010

Oslo, Norway

Serikali ya Tanzania isitishe mpango
wa ujenzi wa barabara
kupitia Serengeti

Mamilioni ya nyumbu na pundamilia wakivuka mto Mara kila mwaka.

Kila mwaka, huvuka zaidi ya nyumbu milioni moja kwenye mto Mara kati ya Serengeti nchini Tanzania na Masai Mara Kenya, pamoja na mamia ya maelfu ya punda milia na swala nusu milioni - wakifuatiwa kwa karibu na simba, fisi na chui. Eneo hili "ni la saba la maajabu ya dunia”, na ni sehemu pekee duniani iliyobaki yenye uhamiaji wa wanyamapori kwa wingi duniani.

- Hii ni dhahabu barani Afrika, na rasilimali kubwa kwa ajili yaTanzania. 

“Kwa sisi tunaofanya kazi maeneo ya upande wa Kenya, tunaona jinsi hili  linavyoongeza ajira" anasema mkurugenzi wa mawasiliano Ole Bernt Frøshaug kampuni yakusafiri Basecamp Explorer kwenye VG Nett.

Kampuni hiyo inaendesha “Eco Hotel Basecamp” Masai Mara nchini Kenya, kwenye maeneo ya hifadhi ambayo ni karibu na Serengeti, Tanzania. Mwaka 2009 National Geographic, imeitaja Basecamp Masai Mara, kuwa ni moja ya kambi  10 bora zilizoko kwenye maeneo ya savannah duniani.

Serikali ya Tanzania ina mipango ya kujenga barabara kuu mpya kutoka mji wa Arusha hadi mji wa Musoma ulio kwenye ziwa Victoria. Barabara hii itakatiza katikati kwenye mbuga ya taifa ya Serengeti. Maeneo haya ndiyo pekee yenye wanyamapori wengi kwenye bara la Afrika. Serikali ya Tanzania inasema kuwa sababu za kutaka kujenga barabara hiyo kubwa itakayokatiza kwenye mbuga ya Serengeti, ni kuwa itarahisisha usafiri kati ya miji hiyo mikubwa, itaunganisha mikoa ya kanda ya kaskazini na itawezesha kukua kwa uchumi kwenye maeneo itakayopita barabara hiyo.

Eneo hili ambalo barabara hiyo inayotarajiwa kupita, linaitwa Hifadhi ya Mara Naibosho na lina hekta 20,000.

 “Sisi tunaofanya kazi upande wa Kenya, tumeaajiri watu 800, na tunaona ni mawazo finyu sana kwa kujenga barabara kwenye vijiji vilivyoko kwenye maeneo ambayo yanayotegemea uchumi wa sekta ya utalii na tunaona barabara inayotarajiwa kujengwa itaharibu uchumi wa wakazi wa vijiji hivyo”. Anasema bwana Ole Bernt Frøshaug, mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya Basecamp Explorer.

Wapinzani wa mpango wa ujenzi wa barabara hiyo wanahofia uharibu wa mazingira na ikolojia  yatakayosababishwa na ujenzi wa barabara hiyo.

Wiki iliyopita kundi moja la wanamazingira barani Afrika, limeishtaki serikali ya Tanzania ili isitishe ujenzio wa barabara hiyo, ambayo ujenzi wake  sio tu kama utaathiri mazingira na ikolojia kwenye mbuga ya Serengeti, bali hata nchi za jirani.

Kuna shinikizo kubwa kutoka kwa wadau wa Tanzania, mashirika ya kimataifa, nchi za jirani na Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Tanzania kiasi ambacho inasadikiwa kuwa serikali ya Tanzania  ina mpango mbadala wa kuipitisha barabara hiyo kusini ya mbuga ya serikali.

”Ujenzi wa barabara barabara hiyo si pekee utakaosababisha uharibu wa mazingira na ikolojia kwenye mbuga hiyo, ukataji kiholela wa miti na uvunaji wa miti ya magogo, ongezeko la watu kiholela pia vitasababisha uharibifu mkubwa sana kwenye eneo hili la saba la maajabu duniani na lazima serikali ya Tanzania ipange mikakati maalumu na madhubuti ili kuhakikisha haya yahatokei” Alimalizia Bw. Frøshaug.

Imetafsiriwa na Mwamedi Semboja, kutoka kwenye makala iliyoandikwa na Stian Eisenträger kwenye gazeti la kila siku la Kinorwe, Verdens Gang (VG) la hapa Oslo, lililochapishwa Jumapili, 26 Desemba 2010.

1 comment:

Anonymous said...

Jamani kuhusu hili, nasema kupanga ni kuchagua. Sababu zinazotolewa zinaegemea zaidi upande mmoja wa biashara ya utalii na kwa kiasi kikubwa ni wenzetu wa nchi Jirani. Nikweli inaweza ikaonekana kama ni upuuzi na ujinga kwa Tanzania kuendelea na uamuzi huo, lakini kwa upande mwingine, tunaweza kuhoji kwa nini ni tanzania tu? nenda south Africa, Botswana hata huku Marekani kwenye mbuga zao, mbona kuna barabara za lami, pili, hivi unaijua adha ya watu wa Musoma linapokuja suala la usafiri. Nadhani ni kutokana na ukweli kwamba wangependa tuendelee kupitia kenya, tatu: There is no way tunaweza kuzuia mabadiliko ya mazingira kwa kungangania kilomita 50 zinzodaiwa. Uwingi wa watalii tayari umeshachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha hiyo ecologia inayodaiwa, nne; tanzania tumejitolea mengi sana, ukombozi, vit ya iddi amini nk, lakini nini tulichoambulia. Mateke; tano; wenzetu wakenya wanajenga uwanja wa ndege wa kimataifa kilomita yapata 60 kutoka ulipo uwanja wetu wa KIA, ni nini kama siyo kumiliki na ikiwezekana kuua KIA kabisa. zipo sababu nyingi. nadhani tuendelee na ujenzi bila woga na tashwishwi.

Wasalaam