Friday, December 10, 2010

Uozo wa mikahawa na mahoteli
ya wageni hapa Oslo

Mamlaka ya usalama wa chakula Norway (Mattilsynet/ Norwegian Food Safety Authority) majuzi imefanya msako mkubwa wa kushtukiza kwenye mikahawa na mahotelini hapa Oslo. Mikahawa na mahoteli mengi imekutwa na pungufu za kanuni za afya na bahati mbaya, mikahawa na mahoteli yaliyobambwa yanamilikiwa na watu wenye asili ya kigeni. Hapo chini ni  baadhi  ya picha zilizopigwa na mamlaka kwenye msako huo.

Nyama ya kuku iliyoingizwa kinyemela toka Sweden, imehifadhiwa kwenye sinki chafu kinyume na kanuni za afya.

Kuku wa kuingizwa kinyemela toka Sweden wamekutwa wako sakafuni wamehifadhiwa kwenye mfuko wa plastiki.

Boksi la kuhifadhia chakula limekutwa chafu na limeharibika

Makabechi yamekutwa yameoza yakiwa sakafuni.


No comments: