Hawa inawezekana waliwekewa vidonge vya kulevya! Hii inatokea sana hapa Norway. Wasichana/wanawake wengi wamekuwa wakiwekewa vidonge vinavyoitwa vya kubaka au Rhyphonol (date rape drug) kwenye vinywaji vyao wanapokuwa “out” au kwenye "party" na ghafla bin vuu wanakuwa hawajitambui, wanachukuliwa na kwenda kubakwa! Ushauri unaotolewa kila mara ni kuwa, ukienda “out” au kwenye "party" peke yako au na wenzako, usije ukaacha kinywaji chako na kwenda kijisehemu na kurudi. Hakikisha kuwa wakati wote macho yako kwenye kinywaji. Ukiondoka, ondoka na glasi yako. Kama uliisahau, ukirudi, mwaga hicho kinywaji na nunua kingine! Hakikisha kuwa unaenda “out” na hata kwenye "party" na marafiki zako na si peke yako.Ukiamua kwenda peke yako, kuwa mwangalifu!
Soma zaidi kuhusu "date rape drug"
Ufirauni ndiyo neno linaloweza kubeba tafsiri ya tukio la mwanamke mmoja (jina kapuni), kutendwa ‘kitu mbaya’ na kijana ambaye hajafahamika. Mwanamke huyo aliyejitambulisha kuwa ni mke wa mtu, alitendwa ‘unyambilisi’ kwa pamoja na mdogo wake ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.....bofya na soma zaidi>>>>>
2 comments:
Hii imetokea kwa rafiki yangu mmoja hapa Oslo msichana wa Kinaijeria. Nilikuwa naye kwenye party. Wakaja jamaa tunawafahamu. Kati ya hao jamaa, mmoja alikuwa ni kama mjombaake. Kwa vile tulikuwa tunawafahamu basi hatukuwa na wasiwasi. Tukawa tunajirusha tu. Kufika wakati wa kutoka, yule mjomba wa shoga yangu akampa lifti. Jamaa alikuwa na rafiki zake wawili. Akampeleka hadi nyumbani kwake. Sijui nini kilitokea, lakini wakaamua kuwa na natchspiel. Si walimwekea hivyo vidonge vya kubaka. Alishtuka asubuhi kaaharibiwa. Kesi ilifika mahakamani na jamaa walifungwa miezi 21 wote watatu.
Jamani tujihadhari tukienda out au kwenye party!
Kibaya zaidi, mtu aliyekuwa anamheshimu kama mjombaake ndiye alikuwa kinara mkuu kwenye kumbaka!
Post a Comment