Mmasai azua kizaa zaa kambi ya Miss Kisura
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mshiriki mmoja wa fainali za Miss Kisura Tanzania 2011, Kipoyane Laibon, kutoka mkoani Arusha, ameripoti kambini hapo akiwa sambamba na mumewe.
Akizungumza na Sufianimafoto, Mumewe huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa ameamua kumsindikiza na kuwaomba wahusika ili kupatiwa mahala pa kulala na mkewe huyo ikiwa ni moja ya kumlina mkewe na kudumisha mila za kwao.
Mumewe huyo aliyeongozana na Kaka wa mshiriki huyo, muda wote walionekana kambini hapo wakiwa na vijifurushi vyao wakiwa nje ya Hoteli hiyo waliyofikia warembo hao wakisubiri muafaka.
Kana kwamba hawakujua kinachoendelea kuhusu mashindano hayo na taratibu zake, mume huyo na Kaka wa mshiriki huyo, walithibitisha hayo wakati wakihojiwa na Sufianimafoto, pamoja na waandishi waliohudhulia uzinduzi wa kambi hiyo leo.

Mume na kaka wa mshiriki wakiwa nje ya hoteli wakisubiri
taratibu za kuambiwa kuhusu mshiriki wao.
Naye mrembo huyo akionyesha ishara ya upole uliopitiliza wakati akihojiwa na kujibu kwa kilugha huku akifinyafinya kucha zake, alisema kuwa, amefika mahala hapo kushiriki shindano la JITAMBUE KISURA, lakini hakuzoea kuwa mahala bila mumewe na ndiyo maana wameamua kusindikizana.
1 comment:
Hii ni changamoto kwa wa-Tanzania. Mashindano ya urembo yamekuwepo katika maisha ya binadamu duniani kote, kwa kila watu kutumia mila, desturi, na vigezo vyao. Hata katika makabila yetu, mila hizi zilikuwepo, kwa kutumia vigezo vya asili, si vya kuigwa.
Sasa mrembo wa ki-Masai amekuja kama hivyo. Tuone mtafanya nini, nyinyi wa-Tanzania ambao mmekuwa hodari wa kuiga mambo, wala hamsomi mawaidha ya watu kama Frantz Fanon, ambao waliongelea masuala hayo kwa ufasaha.
Ushauri wangu ni kwamba, kitu cha kwanza mpeni mchumba na kaka mtu sehemu ya kulala. Watawashangaeni sana, kwamba hamna ustaarabu wa jadi wa kukaribisha wageni.
Post a Comment