Monday, April 18, 2011

Ubalozi wa Marekani watangaza aina mpya ya miadi (appointment) ya huduma za Viza TANZANIA


Kuanzia Ijumaa, Aprili 15, 2011, Ubalozi wa Marekani hapa Dar Es Salaam utaanzisha mchakato mpya ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika kushughulikia maombi ya viza. Maelezo yote katika hili tangazo yanapatikana pia katika tovuti ya ubalozi, Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.

Juu ya mchakato mpya, waombaji wataweza kuchagua miadi kwa ajili ya viza za muda mfupi kupitia tovuti mpya CSC Visa Information Service au kwa kupitia msaada kwa kupiga namba ya kituo cha huduma za wateja             +255-22-2194300 begin_of_the_skype_highlighting            +255-22-2194300      end_of_the_skype_highlighting       ( kwa Tanzania), au            +1-703-439-2304 begin_of_the_skype_highlighting            +1-703-439-2304      end_of_the_skype_highlighting       (kwa Marekani), au kwa kupitia huduma ya Skype ID: usvisatanzania. Waombaji watalazimika kufanya malipo ya visa kupitia huduma ya Airtel Money (ZAP) au Citibank Tanzania Limited iliyopo Peugeot House, 36 Upanga Road, Dar es Salaam) KABLA ya kufanya miadi (Appointment). 

Mchakato huu mpya, unasimamiwa na CSC visa information Services, unategemewa kuleta ufanisi na kurahisisha hatua za uombaji wa viza. Mchakato huu mpya wa maombi ya viza unachukua nafasi ya ule wa zamani. 

Kupitia Mchakato huu mpya, wasafiri watalazimika kuuliza habari zote zinazohusu aina zote za viza, mahitaji yake na hatua zake muda wowote kupitia tovuti: CSC Visa Information Service au kwa kupiga simu mida ya saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili kamili jioni (08:00am-06:00pm) kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kupitia namba             +255-22-2194300 begin_of_the_skype_highlighting            +255-22-2194300      end_of_the_skype_highlighting       ( kwa Tanzania), au            +1-703-439-2304 begin_of_the_skype_highlighting            +1-703-439-2304      end_of_the_skype_highlighting       (kwa Marekani), au kupitia Skype ID: usvisatanzania. Huduma zote zitapatikana na kutolewa kwa lugha ya kingereza tu. 

Kuambatana na mabadiliko haya, Zingatia yafuatayo: 

Kuanzia Ijumaa, Aprili 15, 2011, waombaji wote lazima wajaze maombi yao ya visa (DS160) na lazima kulipia gharama za maombi KABLA ya kuchagua siku ya miadi (scheduling appointment). 

Waombaji ambao walilipia gharama za maombi ya viza (application fee) kabla ya tarehe Aprili 8, 2011, lakini hawakuchagua siku ya miadi (appointment date) kwa ajili ya mahojiano ya viza, NI LAZIMA wafanye hivyo kabla ya tarehe Aprili 28, 2011. 

Malipo ya viza hayawezi kuhamishwa na kutumiwa na mtu mwingine. Malipo ya gharama za viza yataunganishwa na namba za pasipoti ya mwombaji na hayawezi kutumiwa na mtu mwingine yoyote. 

Asante kwa ushirikiano na uelewa wenu katika kipindi hiki cha mpito kuelekea huduma bora za mambo ya viza hapa katika ubalozi wa Marekani. Ni mategemeo yetu kwamba huduma hii mpya itaongeza huduma bora za viza kwa wateja. 

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma hii yatawekwa katika tovuti yetu: Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.


Article translated in:
English

No comments: