Malalamiko ya Watanzania waishio Saudi Arabia
SISI Watanzania tunaoishi Saudi Arabia kikazi, kimatembezi na kimaisha, tunayo majonzi na masikitiko makubwa kuhusiana uhusiano usioridhisha baina yetu na ofisi ya ubalozi wetu nchini hapa, hali ambayo imetuvunja nguvu na kupoteza mategemeo na mafanikio na malengo yetu ya kuinua hali na maendeleo ya nchi yetu Tanzania.
Tupo hapa Saudi Arabia kwa malengo ya kuitangaza nchi yetu katika nchi za Kiarabu na duniani kote, juhudi ambazo zinazaa matunda kwa kikubwa.
Tukirudi nyuma kidogo, tulifurahishwa sana na ziara ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, na viongozi wengine wa serikali nchini Saudi Arabaia ambayo ilifanyika Aprili 14, 2009 hadi Aprili 17, 2009.
Katika kipindi hicho kifupi cha siku tatu, ziara hiyo ilitangaza zaidi jina na picha ya Tanzania katika nchi hii ambapo alitembelea sehemu nyingi za miradi mbalimbali ya kibiashara na akakutana na viongozi mbalimbali wa Saudi Arabia akiwamo Prince Alwaleed bin Talal bin Abdul Aziz al Saudi, na viongozi wengine nchini hapa.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuwavuta wawekezaji na wafanya biashara wa kimataifa kuwekeza miradi yao nchini Tanzania.
Mwisho wa ziara hiyo, Rais Kikwete na ujumbe wake alikutana na jumuiya ya Watanzania walioko nchini Saudi Arabia, jambo ambalo lilitutia moyo na kutujaza furaha kubwa.
Kama ilivyotegemewa, wawekezaji na wafanyabiashara wa hapa walimiminika katika ubalozi wetu hapa jijini Riyadh kuitumia fursa iliyotangazwa na Rais Kikwete. Ubalozi huo uliwapokea na kuwasaidia ipasavyo, japokuwa haikuwa na balozi kamili aliyekuwa ameteuliwa huko nyumbani kushika wadhifa huo.
Lakini mambo yamebadilika baada ya kuwasili kwa balozi mpya hapa, jambo ambalo limewafanya wafanyabiashara wengi wa kigeni waliokuwa na nia ya kuwekeza mitaji yao nchini Tanzania, kuka safari zao ghafla. Hii ni kwa sababu balozi mpya amekuwa ni mtu asiyekuwa tayari kuwasiliana na watu wanaopeleka matatizo yao kwenye ofisi yake.
Jambo hili limetukera sana sisi Watanzania na watu wengine wanaotaka kuwasiliana na ubalozi huo.
Mfano mmoja wa hali hii mbaya ni kwamba pamoja na Watanzania walioko hapa kujitolea michango mara mbili kuandaa chakula mkono wa kumkaribisha na kutambulishana kati yetu na yeye binafasi, balozi huyo anaonekana amekataa kukutana na sisi.
Katika safari zote hizo mbili amekuwa akiwatumia maofisa wa chini yake badala ya kufika yeye mwenyewe.
Hivi sasa umetimia mwaka hatujakutana naye na kubadilishana naye mawazo. Hivyo, hali hii inatupa mashaka kwani juhudi zetu za kutaka kuitangaza nchi yetu na kuchangia maendeleo yake, zinaonekana kukwama.
Tunaomba zichukuliwe hatua za makusudi kutatua tatizo hili linalotaka kuziba njia yetu ya kuiletea ustawi nchi yetu.
Jumuia ya Wantanzania,
Saudi Arabia.

No comments:
Post a Comment