Monday, May 23, 2011

Mwisho wa kuchungulia mapato ya rafiki, jirani, ndugu na jamaa!


Serikali ya Norway, imeamua kuzuia orodha ya mapato ya watu, kuwekwa wazi kwenye vyombo vya habari. Vyombo vya habari vitapewa orodha ya mapato ya wakazi wote waishio Norway, lakini havitaruhusiwa kuchapisha.

Kuanzia mwakani, mtu ambaye atataka kuchungulia mapato ya jirani, rafiki, ndugu au jamaa itabidi aipitie kwenye mtandao wa serikali MinID kwa kutumia tarakimu zake 11 za utambulisho (National Identity Number). Na mtu utakayemchungulia atapata taarifa kuwa umeingia na kuchungulia mapato yake.

2 comments:

Anonymous said...

Patamu hapo.How about phone numbers.Mbona wambea wamjini wameumbuka na hizi free internet connection walizidi.Watajicarry live

Anonymous said...

Hapa ujanja hakuna. Ukiingia kunichungulia nitajua na nitakuuliza kulikoni kunifuatilia fuatilia?