Thursday, June 23, 2011

Polisi wa Sweden: Picha ya Mfalme Carl Gustaf akiwa kwenye baa ya wacheza uchi

Mfalme Carl Gustaf wa Sweden


Habari za kuaminika kutoka kwenye gazeti la Expressen la Sweden, zinasema kuwa polisi wa nchi hiyo wana ushahidi wa picha inayomwonyesha Mfalme Carl Gustaf akiwa kwenye klabu ya wacheza uchi.

Kama wiki 3 zilizopita, Mfalme Gustaf akihojiwa na shirika la habari za Sweden TT (Tidningarnas Telegrambyrå) , alikana na kusema kuwa hakumbuki kama amewahi kukanyaga kwenye klabu za namna hiyo.

Ijumaa 18.Juni, polisi wa Stockholm walimkamata jamaa mmoja aliyekuwa anamiliki klabu za wacheza picha za ngono, Mille Markovic na kuchukua kompyuta yake, simu zake za viganja na kalamu za kuhifadhi data (memory stick) zake. Polisi wanasema kwenye “memory stick” moja wamekuta picha ya Mfalme Gustaf akiwa kwenye moja ya klabu zilizokuwa zikimilikiwa na Markovic.

"Gangstar" Mille Markovic

Markovic alikamatwa akiwa njiani akielekea Serbia (ana asili ya Serbia), walimwachia Jumamosi 18 Juni.

Markovic (49) ni chanzo kwenye kitabu kinachoitwa «Carl XVI Gustaf - Den motvillige monarken» kilinachoelezea jinsi Mfalme Gustaf alivyokuwa anaishi maisha ya raha, kunywa na kutembelea mabaa usiku, bila ya malkia kujua nini kinatendeka.

3 comments:

Anonymous said...

Duh! Mfalme kaongopa na sasa anaumbuka!

Anonymous said...

Lakini jamani yeye si kama binadamu wengine wote? Au kwa vile ni Mfalme basi tena...kama ni hamu za ngono anazo kama wanaume wengine...mwacheni Mfalme Gustaf

Anonymous said...

ndio mijanaume ilivyo most of them anyway hamridhiki.Na we anon ndio walewale kama ana hamu za ngono,whaaat ?