Saturday, July 16, 2011

Malkia wa Swaziland afungiwa ndani mwaka mzima sasa baada ya kufumaniwa akiwa anakula uroda na waziri wa sheria

Mfalme Mswati III wa Swaziland 

Malkia Nathando Dube (23) 

Malkia na Mfalme.

Mfalme Mswati III wa Swaziland amemfungia ndani Malkia Nathando Dube (23) mwaka mmoja sasa baada ya kumfumania kwenye hoteli ya Royal Villas nje kidogo ya mji mkuu wa Mbabane akila uroda na waziri wa sharia wan chi hiyo; Ndumiso Mamba.

Malkia Nathando alifumaniwa na walinzi wa Mfalme Mswati baada ya kuhisi kuna kitu kinatendeka kati ya Malkia na waziri wa sheria.

Baada ya kufumaniwa, Malkia amefungiwa ndani kwa mwaka mzima, bila ya kuonana na Mfalme wala familia yake. Malkia amezaa watoto watatu na Mfalme. Mtoto wa mwisho ana miezi 14.

Malkia Nathando akiwa na miaka 16 alikutana na Mfalme Mswati kwenye moja ya hafla za Mfalme na Mfalme akavutiwa na Nathando na baada ya muda akaolewa na kuwa Malkia.

Uvumi umeenea kuwa baada ya kufumaniwa, waziri huyo wa sharia amenyongwa kimya kimya, lakini msemaji wa Mfalme Mswati amekataa kuthibitisha au kukataa kuhusu uvumi  huo kwenye gazeti la Mail & Guardian la Afrika Kusini.


No comments: