Saturday, July 30, 2011

Mmmh na wanene Bwana! Hata wakinasa, kazi yao kushambulia tu..


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,

Uzitoni Street,

Bongo.
Mpenzi Frank,Unajua wenzako walikupigia picha ukiwa umelala fofofo juu ya benchi? Na wamenitumia? Unataka kuiga vya wanene? Wacha hizo mpenzi wangu. Wengine wanalala shauri ya shibe, wewe shauri ya njaa teh teh teh. Iga ufe nakuambia maana wao wanalipwa posho za kulala, wanalalia posho, wewe utalipwa posho gani?

Lakini pole mpenzi. Najua kutembea mji mzima kila siku ni kazi kubwa. Siyo sawa na kukalia masponji huko. Labda na wanene wangeondolewa masponji yote hayo wasingeshambuliwa na usingizi wa aibu namna hiyo.


Bofya na endelea>>>>

No comments: