Monday, July 18, 2011

Ndege ya kivita aina ya Sukhoi 
Su-30MK2 ya jeshi la anga la Uganda

Hii iliruka mara ya kwanza kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe, 13 Julai 2010.


Uganda wamenunua ndege sita za kivita za aina ya Sukhoi Su-30MK2. Uganda ni moja ya jeshi la anga lenye ndege za kisasa barani Afrika. Ni tishio kwa nchi za Afrika Mashariki, kwani Kenya na Tanzania zina ndege za kivita zilizobuniwa miaka 50 iliyopita.

Sukhoi SU-30, inajulikana kama Flanker kwa nchi za NATO, ziko modeli mbali mbali. Iliingia kwenye jeshi la anga la Urusi mwaka 1996. Ina kasi ya Mach 2.0 (2,120 km/h, 1,320 mph) na ni ya kisasa au kwa msemo mwingine ni “4.5 Generation of Fighter Jets”. Flanker inafananishwa na Eurofighter Typhoon na F-15E Strike Eagle ya Marekani. 


3 comments:

Anonymous said...

Na hizi Sukhoi zao, Waganda wakitaka watakuwa wanafanyia mazoezi kwenye anga ya Tanzania bila ya rada yetu kujua kuwa Su-30 ziko wapi na marubani wetu watakaporuka na MiG-21 au MiG-19 zetu toka Ngerengere au Mwanza, zamani watakuwa wamerudi wako Entebbe. MiG-19 au MiG-21 zikijifanya kujua, zitatunguliwa bila hata kujua nini kimetokea. Tuwaombe Wachina watuuzie Chengdu J-10 hizi ndizo zinaweza kukabiliana na Su-30

Anonymous said...

Twafaaaaaaaa!!!!

geofrey andrew sanga said...

tuombe mungu m7 asigeuke iddi amin maana sisi nyerere alikufa na sasa wamebaki mafisadi na walinunua rada mbovu na chenji wanatupiga chenga wakati akina brown wamesema tukachukue.