Sunday, August 28, 2011

Baada ya kuiba simu, ikipigwa simu yaita tumboni, baada ya dakika 10 tumbo lake huvimba!


 Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara eneo hilo baada ya wiki moja simu hiyo imekuwa ikilia tumboni baada ya kupigwa huchukua kama dakika kumi na tumbo lake kuvimba. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.

Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.

Kijana GOODSON ni mmoja wa wafanyakazi wa Machinjioni maarufu kama Butchery Mbalizi.

No comments: