Wednesday, September 07, 2011

Blogu ya Ikulu Tanzania kunani?
Jamani hivi blogu ya Ikulu inaendeshwaje?Habari za mwisho ni za 25 Machi 2011. Kuna mtu anaweza kuwasiliana nao wawe wanatoa habari za kila siku? Nimewaandikia mara kadhaa, lakini mapaka leo sioni mabadiliko yoyote! Sijui hata wanasoma barua pepe za maoni ya watu!

Ikulu ina kurugenzi ya mawasiliano, kwa nini kurugenzi inashindwa kutoa habari za kila siku kwenye blogu yao?

Mdau,
Tausi Usi Ame Makame.

6 comments:

Anonymous said...

Hii inatoa picha jinsi gani nchi ya Tanzania inavyoendeshwa!

Mzalendo wa nchi said...

Kuna Salva Rweyemamu kwenye kurugenzi ya mawasiliano sasa sijui vipi anaichukuliaje hii blogu. Labda umri na teknolojia hii vitu vinamshinda. Bora wamwachie Issa Michuzi aiendeshe hiyo blogu

Mzawa said...

Mzalendo umenena. Bora wamwachie Michuzi aisimamiehiyo blogu ya ikulu. Kina Salva Rweyemamu wameshindwa kazi......

Anonymous said...

Wanipe mimi kuiendesha hiyo blogu

Anonymous said...

Wamwachie tu Michuzi hiyo blogu

Anonymous said...

Si lazima Michuzi, kuna wengi vijana wanaweza kufanya kazi hiyo wakisaidiwa na Michuzi kama mshauri wao