Thursday, September 15, 2011


MV Spice Islanders ilibeba abiria 3,000


Elias Msuya na Jackson Odoyo, Zanzibar

MELI ya MV Spice Islanders iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya takriban watu 200 na majeruhi 619 ambao waliokopolewa, ilibeba abiria 3,000 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 600 tu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa idadi hiyo kubwa ya abiria, haijumuishi mizigo ambayo kiasi chake bado hakijajulikana.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Fakhi Dadi alisema jana kuwa mkoa huo umepoteza watu 1,600 katika ajali hiyo, huku Wilaya ya Wete pekee ikiwa imepoteza watu 1,141.Dadi alisema hayo alipokuwa akizungumza mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif HamadNo comments: