Sunday, September 18, 2011

Nedre Romerike

Mcheza mpira aanguka na kufariki uwanjani.Sherehe za kufurahia uwanja mpya wa mpira wa timu ya Høland, ziliishia kwa masikitiko. Wapenzi 200 wa timu ya Høland wilayani Nedre Romerike walifika kwenye uwanja huo mpya wenye nyasi bandia kuangalia mazoezi ya timu hiyo. Mazoezi hayo yalikuwa ya wachezaji wakongwe waliochezea timu hiyo kwenye miaka ya 80 na 90.  Baada ya dakika 20, mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 40 alianguka kwa kushikwa na ugonjwa wa moyo ghafla na kufariki hapo hapo uwanjani. Helikopta ilifika hapo haraka na daktari na wahudumu wengine na kujaribu kuokoa maisha ya mchezaji huyo, lakini ilishindikana.

No comments: