Thursday, September 22, 2011

Porphyry (Rohmbporphyry) - Mawe yanayopatikana maeneo matatu tu duniani, nayo ni: Oslo, Antaktika na kwenye mlima Kilimanjaro



Jana nikiwa na darasa langu tulitembelea shule ya Sørkedalen iliyopo maeneo ya Sørkedalen, Manispaa ya Bærum (Baerum) kwenye mpaka kati ya mkoa wa Oslo na Buskerud. Madhumuni ya safari  - kutembea kilomita 3 msituni kwa kutumia ramani na dira na kupika kwa kutumia nyenzo za mapishi za kiasili za Kinorwejiani.

Niliokota jiwe hili. Wanajiolojia wanaliita liitwalo Porphyry.

Jiwe hili linapatikana maeneo matatu  tu duniani: Maeneo  ya kuzunguka Oslo, kwenye mlima Kilimanjaro, na kwenye kontineti la barafu la kusini ya dunia (Antaktika).

Mwamedi Semboja,
Oslo.

No comments: