Thursday, September 01, 2011

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ziarani Norway

Rais Jacob Zuma akiwa na mkewe wakiwa na Mfalme Harald V wakishangiliwa na watoto kwenye hekalu la Mfalme (Slottet). Picha kutoka: www.kongehuset.no 


Rais Jacob Zuma yuko kwenye ziara ya siku mbili nchini Norway. Rais Zuma yuko nchini kwa mwaliko wa Mfalme Harald na Malkia Sonja (inatamkwa Sonya), kufuatia ziara yao ya Afrika Kusini mwaka 2009. Rais Zuma ambaye ana wake watano; kwenye ziara hii amefuatana na mkewe mmoja tu aitwaye; Tobeka Zuma.

Jana aliembelea ngome ya Akershus na kutembelea kanisa la kuu la Oslo na kuweka maua kama kumbukumbu ya watu 77 waliouawa na gaidi Anders Behring Breivik Julai 22.

Baadae, Mfalme Harald na Malkia Sonja walifuatana na Rais Zuma na mkewe hadi makao makuu ya tuzo amani ya Nobel. Taasisi ya tuzo ya amani ya Nobel, imewatunukia tuzo ya amani ya Nobel; kiongozi wa ANC; Albert Luthuli mwaka 1960 (Mwafrika wa kwanza kupata tuzo ya amani ya Nobel), mwaka 1984, Askofu Desmond Tutu na mwaka 1993; Nelson Mandela na Fredrik de Klerk.

Leo hii; Rais Zuma na mkewe Tobeka watakuwa kwenye maakuli rasmi kwenye hekalu la Mfalme Harald mjini Oslo.

No comments: