Monday, October 24, 2011


Kweli sisikii

Kuna Mzee alikuwa kila akiweka wine yake akija kuinywa tena anakuta ladha imebadilika! Akaamua weka mtego, siku 1 akanywa wine kidogo akaacha akatoka yeye, mkewe na hausegal wakamwacha houseboy nyumbani, huku nyuma houseboy kama kawa kajipindua kanywa wine kidogo kajaza maji kufidia! Mzee kurudi kuonja wine akaanza kufoka house boy kuona vile akakimbilia banda la kuku! Mzee ita sana "Wee Juma, Juma!" houseboy kala bati! Mzee na mkewe wakaenda hadi banda la kuku!

Mzee: We Juma si nakuita wewe!
Juma: Sikusikia mzee!
Mzee: Yaani wewe upo bandani mi naita wajidai hausikii? Inawezekanaje?
Juma:Kweli baba ukiwa bandani husikii mtu akiita! Kama wabisha ingia uone!
Kweli Mzee akaingia Juma akabaki nje, Juma akaanza payuka "Eti Baba nani anatembea na Housegirl humu ndani?" Mzee kimya! "Baba nauliza nani anatembea na Housegirl?"

Mzee akatoka kweli Mwanangu kumbe ukikaa humu usikii kitu!
Haya kaendelee na kazi Mwanangu!


Kutoka kwa mdau,
Jamaldeen Mazar E Shariff Bin Ad-Din Vituz Mamluk Ibn Zenjibari

No comments: