Friday, October 21, 2011

Orodha ya kodi imetolewa leo


Orodha ya walipa kodi wote wa Norway imeshawekwa mtandaoni. Unaweza "kumchungulia" jirani yako, ama ndugu na jamaa ujue mwaka 2010 alichuma kroner ngapi na alilipa kodi kiasi gani!!!!! Hapa Norway orodha kama hizi zimekuwa zinamwagwa waziwazi watu wajionee.

Watu wengi wamekuwa wakipinga kuwekwa kwenye kadamnasi orodha ya walipa kodi. Walalahoi na walalahai wanasema kuwa nani anachuma kroner ngapi na analipa kodi kiasi gani kwa mwaka ni masuala ya binafsi hivyo hayapaswi kujulikana na umma wote wa ndani na nje ya nchi.

Mwaka huu mtu hawezi kumtafuta jirani, ndugu, jamaa au rafiki hivi hivi tu. Lazima uingie kwenye

 au

Halafu ndio unaweza kuchungulia, lakini mtu unayetaka kumchungulia anapewa taarifa kuwa unataka kumchungulia taarifa zake za mapato na kodi!!!
 
Norway ni nchi pekee duniani "inayoanika" orodha ya walipa kodi.

No comments: