Tuesday, November 01, 2011Aftenposten, Jumapili, Oktoba 30.
Norway haitaki kujua undani wa hela zao za misaada Tanzania zinatumikaje:

Ukurasa wa mbele wa Aftenposten, Jumapili Oktoba 30

Ukurasa wa 6 na 7, Aftenposten, Jumapili Oktoba 30


Makala mfululizo kwenye gazeti la kila siku hapa Norway la Aftenposten, ikiendelea kwenye toleo la Jumapili tarehe 30 Oktoba. Aftenposten wanaulizia kwa nini serikali ya Norway, licha ya ripoti za ubadhirifu na ufisadi wa hela zao za misaada nchini Tanzania, inashindwa kufuatilia jinsi gani serikali ya Tanzania inazishughulikia ripoti hizo.

Mkaguzi mahesabu maarufu hapa Norway; Bw. Einar Døssland wa kampuni ya ukaguzi ya Faktum Nor AS amepitia ripoti tatu za ukaguzi ambazo ubalozi wa Norway nchini Tanzania uliagizia ili kujaribu kujua nini kinaendelea. Kinachoshangaza ni kuwa serikali ya Norway imeridhika na kurudishiwa kroner 750 000 (laki saba na hamsini elfu) tu kati ya kroner 150 000 000 (milioni mia moja na hamsini) zilizopotea kimiujiza ujiza! Kwenye mradi wa MNRP.

Døssland anashangazwa na ukimya wa serikali ya Norway wa kutoiwajibisha serikali ya Tanzania kwenye suala hili. Anasema kuwa ubalozi wa Norway mjini Dar es Salaam umeipa TAKUKURU (PCCB = Prevention and Combating of Corruption Bureau) vielelezo na vidhibiti dhidi ya ubadhirifu kwenye mradi wa “Management of Natural Resources Programme = MNRP” lakini ubalozi wa Norway na serikali ya Norway vimeshindwa kufuatilia kwa makini kuwa TAKUKURU wamefikia wapi kwenye hili. Ubalozi wa Norway na serikali ya Norway zimekuwa zikisikiliza zaidi serikali ya Tanzania juu ya kesi hiyo; huku zikijua fika kuwa serikali ya Tanzania haisemi ukweli juu ya skendo ya MNRP.Aftenposten, Jumatatu, Oktoba 31.
NORAD inapaka vipodozi ripoti zao za mwaka kwenye skendo ya misaada inayotolewa Tanzania:


Ukurasa wa 8 Aftenposten, Jumatatu Oktoba 31.


Kwenye makala inayoendelea juu ya ubadhirifu kwenye hela za misaada zinazotolewa kwa Tanzania; gazeti la Aftenposten linaandika kuwa; shirika la misaada la Norway; NORAD linapaka vipodozi ripoti zao za mwaka kwenye hela za misaada zinazotolewa kwa Tanzania.

Kwenye ripoti  za NORAD za mwaka 2006, 2007, 2008 na 2009, hakuna hata sehemu moja inayoelezea kwa undani hasa juu ya ubadhirifu kwenye mradi huo wa “Management of Natural Resources Programme”.

Mwaka 2009 jarida moja “Development Today = DT” liliiomba NORAD (NORAD iko chini ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Norway) kuipitia ripoti ya Baker & Tilly inayohusu ukaguzi wa miradi  ya Norway Tanzania; lakini wizara ya mambo ya mambo ya nchi za nje hapa Oslo; ilikataa ombi la Development Today”. Baada ya DT kukata rufaa, ndipo wizara ikaitoa ripoti hiyo ikiwa imekatwa katwa sehemu kubwa.

Hii inaonyesha kuwa Norway inajua fika wapi na nani kachota hela hizo; lakini imeshikwa na kigugumizi. Au wadau wengine wanadai kuwa kuna ufisadi kwa baadhi ya wafanyakazi  wa NORAD. Kama hakuna mafisadi kwa nini basi watie vipodozi ripoti zao kuficha ufisadi nchini Tanzania?


No comments: