Tuesday, November 29, 2011

Upungufu wa siagi

Kumekuwa na upungufu wa siagi hapa Norway kwa takribani wiki mbili sasa. Upungufu huo unahusu sana siagi zinazotengezwa na kampuni ya Tine. Sababu zinazotolewa ni kuwa kumekuwa na uzalishaji pungufu wa maziwa, hivyo kusababisha Tine kushindwa kuzalisha bidhaa zinzotokana na maziwa. Kuna uwezekano upungufu huo ukaendelea hadi kuingia wiki za mwanzoni za mwaka 2012.


No comments: