leo
ni siku ya ukimwi duniani:
tafakari
Leo ni siku ya ukimwi Duniani,
Nimeona nitumie nafasi hii ili tukumbushane na Watanzania wenzangu na
hata walio sio watanzania kwani hili ni tatizo kwa kila nchi na kila jamii hapa
duniani.
Hili tatizo la ugonjwa huu wa ukimwi (AIDS) limetukabili na inabidi
tulichukulie kwa makini na tulipe umuhimu sana kwani limetuathiri sana na
linaendelea kutuathiri kuanzia wazee, vijana na hata watoto katika jamii.
Naomba tuwe mstari wa mbele katika kwenda kupima na kujua msimamo wetu
na vilevile kuwakumbusha watu wengine kwenda kupima na bila kuogopana.
kwa mfano mtu anapopata mchumba basi asisahau kumkumbusha mwenzake
kwenda kupima kwani kufanya hivyo kutaokoa maisha ya wengi hasa ukizingatia
wengi wanaoambukizwa katika jamii yetu wameambukizwa na waume au wake zao kwa
kuogopa kukumbushana kwenda kupima.
Na baada ya kupima utapata ushauri mzuri toka kwa daktari wako katika
jinsi gani ya kujiepusha zaidi hata kama uwe unao ugonjwa au huna.
Katika siku hii ya ukimwi duniani, tumia fursa hii kumkubusha mwenzio
kuhusu hili suala hata kama hataki kusikia lakini yatakuwa yamemuingia akilini.
Naomba kwa mwenye kutaka ushauri zaidi kuhusiana na ugonjwa huu basi
awasiliane nami kupitia.......
Kumbuka sio lazima ujitambulishe kwa jina unaweza kutumia jina lolote
ili kuondoa wasiwasi.
-Buhite Aljabry
No comments:
Post a Comment