Wednesday, December 14, 2011

Marekani yaruhusiwa kuhifadhi taarifa binafsi za wasafiri wote wa ndege kwa zaidi ya miaka 15 ijayo!


Pamoja na upinzani mkubwa kutoka mataifa ya Ujerumani na Austria, mawaziri wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) wameidhinisha makubaliano kuruhusu idara za usalama za Marekani kuhifadhi takwimu binafsi za wasafiri wa ndege kwa miaka 15.

Makubaliano hayo ambayo ni lazima yaidhinishwe na Bunge la nchi za Umoja wa Ulaya, yanatoa haki kwa mashirika ya Marekani kuchambua taarifa kwa muda wa miaka 15 kwa ajili ya uchunguzi unaohusiana na ugaidi.

Miongoni mwa taarifa hizo pamoja na mambo mengine, zinahusu majina ya wasafiri, anwani zao na taarifa zao za kadi za benki.

Vyanzo:

1 comment:

Anonymous said...

Duh! Yaani mataifa ya Ulaya hayana ubavu mbele ya Marekani? Aibu kubwa!