Friday, December 23, 2011Kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko Tanzania


Habari Jumuiya ya Watanzania Oslo

Nimeguswa sana na suala la mvua na hadha iliyosababishwa nayo nchini Tanzania, pia nimeguswa na idadi kubwa ya watu walioachwa bila makazi wala msaada. Nimeangalia ni jinsi gani naweza kuwasaidia watanzania wenzangu na nimeona ni bora nitume barua pepe hii kwa jumuiya zote zilizopo nje ya nchi ili kwa pamoja ziweze kuwakutanisha watanzania na kukusanya chochote kiwezekanacho na kuwepelekea watanzania wenzetu waliopo Tanzania bila msaada. 

Mimi binafsi nipo kusini mwa Ufaransa katika mji wa Toulouse na kwa bahati mbaya sijapata kujua jumuiya wa Watanzania katika mji huu wala Paris na pia sijabahatika kukutana na mtanzania mwingine zaidi ya mmoja ambaye tupo nae pamoja chuo. 

Asanteni na natumai wote tutashikama kwa ajili ya nchi yetu Tanzania.

Mponda Malozo
+33 684 21 45 01
Toulouse, France
Skype: Malozo.
Web: www.unawetanzania.org


No comments: