Tuesday, January 17, 2012

Oslo, Norway

Jichunge kwenye maeneo yafuatayo:


Mkuu wa polisi wa Oslo; Bw. Anstein Gjengedal.


Mwaka jana polisi Oslo walipokea malalamiko 15000 ya watu kuibiwa pochi zao. Jana mkuu wa polisi Oslo; Bw. Anstein Gjengedal alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari. Bw. Gjengedal ameonya watu kuwa waangalifu kwenye maeneo yenye kadamnasi ya watu kama vile kwenye mabasi, matreni ya mjini na kwenye maduka makubwa. Ametaja maeneo kutokea National Theater kupitia mtaa mkuu wa Oslo; Karl Johan, kuelekea Stesheni Kuu ya Treni, Youngstorget, maeneo ya Halmashauri ya mji wa Oslo, maeneo ya Brugata na maeneo ya Majorstuen kuwa ndio yanayoongoza kuwa na vibaka wengi.No comments: