Wednesday, February 08, 2012

Norway


Bei ya petroli inatisha!




Bei ya petroli inatisha hapa Norway. Leo hii, wastani wa bei ya petroli ni kroner 14,83 (15,-) kwa lita kwa petroli ya kawaida. Statoil ndo wa kwanza kupandisha kwa bei hiyo kwenye vituo vyao vya petroli. Msemaji wa Statoi Fuel & Retail Norway, Bw. Pål (Paul) Heldaas amesema kuwa bei ya petroli itazidi kuongezeka siku zinazokuja kutokana na hali ya uchumi ilivyo duniani. Mchumi wa DNB Market; Bw. Torbjørn Kjus, anasema kuwa bei ya mafuta itazidi kuongezeka, kutokana mgogoro kati ya Iran na Marekani na nchi za magharibi utakavyoendelea. Kama nchi za Ulaya Magharibi zitagomea mafuta ya Iran, bei ya mafuta itapanda maradufu.

Jana bei ya pipa moja la mafuta ghafi ilikuwa Dala za Kimarekani 116,-

No comments: