Saturday, March 24, 2012


Majira ya Kiangazi




Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 25 Machi 2012, tunabadili majira na kuingia majira ya Kiangazi (Summer time). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunasogeza saa moja mbele. 

Tuna tofauti ya saa moja na saa za Afrika Mashariki kwenye majira ya Kiangazi. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 5 za asubuhi,

Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.

Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summer). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.
Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Winter). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.



No comments: