Sunday, March 18, 2012Mwalimu Nyerere alipokuwa Rais,  aliwahi kutembelea hospitali ya vichaa ya Mirembe. Akatembezwa eneo la wagonjwa walio karibu kuruhusiwa kwenda kwao, akaanza mazungumzo na mgonjwa mmoja,

Nyerere: Hujambo bwana?
Mgonjwa: Mi sijambo sana
Nyerere: Unanifahamu?
Mgonjwa: Sikufahamu kwani wewe nani?
Nyerere: Mi ndie mkuu wa nchi hii
Mgonjwa: Duh hahahahahaha aise, unajua na mimi nilipofika hapa mara ya kwanza nilikuwa najiita mara Waziri Mkuu, mara Kiongozi mkuu, lakini nashukuru sasa nimepona baada ya miaka 10, ila wewe dah, umesindikizwa na wanajeshi, mapolisi na mapikipiki nadhani wewe utakaa sana humu

No comments: