Thursday, March 29, 2012

Sikiliza matusi - Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - "Matusi yakija nitatukana, hoja zikija nitasema..potelea mbali". "Nataka kuwaambieni..wenzetu wanajifanya wanajua kutukana, hapa mwisho!". "Unajua kuna wabunge wa CHADEMA, maji marefu unawalea sana..wewe ndio uliowachanja chale mpaka matakoni, leo wanakutukana.."Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akimwaga sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Viwanja vya Ngarasero katika Kata ya USA River Wilayani Arumeru. Mkutano huo ulifanyika tarehe 26/03/2012 majira ya saa 9 Alasiri.

10 comments:

Mosi_O-Tunya said...

CCM wanamjua huyu kuwa ni mtu wa aina gani. Hata alipoenda Arumeru walijua fika atazungumza nini.

Inasikitisha.

Sijasikia waliyosema CHADEMA, lakini kama ni kweli, siasa za Tanzania zinasikitisha kweli!

Anonymous said...

Duh! mtu mzima anatukana hivi?

Anonymous said...

Kiongozi kama huyu alipaswa ajibu kwa njia ya hoja ili ionekana CCM imekomaa kisiasa sasa hivi kama ni kweli anavyosema Chadema wanatukana sasa na yeye anatukana sasa wananchi tunawaonaji wote wapuuzi. Inamana mwendawazimu akikupiga wewe utapigana nae wote hamfai kuongoza hii nchi ndiyo maana nchi inaenda inakoelekea.

Tutakula au fitna? said...

Ni kweli ndio maana nchi inakwenda mrama!

Mpenda amani said...

Ni aibu kubwa. Wakati anatoa matusi hayo ni watoto walikuwepo, kauchuna hana aibu hata kidogo. Halafu ni Mbunge huyu? Dah! Sielewi kuwa vyama vya siasa Tanzania vinaweza kutukanana kwa matusi ya nguoni kiasi hiki.

Anonymous said...

Pamoja na matusi yote haya CCM wameshindwa!

MwanaCCM mdemokrasi wa kweli said...

CCM tukae tukijua kuwa kuna vyama vya upinzani makini sasa si mchezo! Tuliwapeleka wazito wao wote tukaogopa kumpelekea mwenyekiti wetu Kikwete manaake ingekuwa aibu.

CHADEMA sasa onyesheni upevu angalieni makosa yenu jisahihisheni na nawatakia kila la heri.

Kama alivyosema Nape Mnauye baada ya matokeo kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Wana CCM tukubali tumezidiwa kete na CHADEMA Arumeru.

Tuwe makini na watu kama hawa wanaotukana saa zote. Ikiwezekana tuwaondoe. Kuna vijana wengi CCM wenye uwezo wa kuzungumza bila kutukana!!!

MwanaCCM Mdemokrasia wa kweli

Anonymous said...

Yaani nashangaa wamama wanatukanwa kwani kupata mimba ni dhambi nao kwakukosa elimu na uelewa wanamshabikia. Hawa ndo watu wanauwa CCM. CCM inakuwa kama chama cha mitaani tu. CCM tutumie akili hapa tunazidi kuivunja badala ya kuijenga. Watu wameeendelea sikuhizi. Mtu anatukanaje kwenye kadamnasi hivyo na kuachiwa huru. Kweli nchi haina sheria ni bora tu wapinzani iwe CAHDEMA au CUF wachukue tu uongozi kurekebisha nchi ime kufa kwishnei. Watu wengi tunajitoa CCM japo hatujui tunaenda wapi lakini kuliko niwe kwenye chama kimajaa matusi hivi bora kutojihusisha na vyama kabisa

Anonymous said...

Waanzishi wa ccm akina Marehemu Nyerere wangesikitika kuona lunateck kama huyu anawakilisha chama chao

Anonymous said...

Mmmmmmh!