Tuesday, March 13, 2012Wizi wa viwanja Tanzania


Nimebanwa na shughuli kwa muda sasa lakini kutokana na suala ambalo limenipata nikiwa Bongo, inabidi nitafute muda na kuomba ushauri kutoka kwenu.

Mtakumbuka wakati tunajadili masuala ya viwanja niliwahi kuwaeleza kuwa kuna mvamizi mmoja (Jack Pemba and Co) ambaye alivamia kiwanja changu (cha familia) mwaka 2006 na kubomoa kibanda ambacho tulikijenga. Yeye alidiriki kuweka foundation yake na ukuta. Tulifanikiwa kumfukuza baada ya kutoa ripoti Polisi na Ardhi na ilipodhihirika kuwa kiwanja ni chetu kutumia records zilizopo Ardhi.

Sasa amejitokeza mvamizi mwingine ambaye ambebomoa msingi wa nyumba tulioweka tena amekuja na court order. Alivyofanya ni kuwa alifungua kesi feki akidai kuwa kiwanja ni chake eti ameuziwa na mdogo wangu. Walivyofanya (nimeambiwa hii ni syndicate ya uporaji viwanja ) ni kuwa walichonga documents za uuzaji waka forge signature ya mdogo wangu na kuzipeleka mahakama ya ardhi Kinondoni. Halafu kesi ikafanyika huku wakidai kuwa mdogo wangu alikuweko kortini wakati yeye wala hakuwa na habari kuwa kuna kesi inamhusu achilia mbali yeye kuwepo kotini.

Kesi ikafanyika, eti mdogo wangu (ambaye wala hakuwepo) akakiri kuwa kiwanja ni cha yule mvamizi kwahiyo apewe. Kwahiyo ikatoka judgement kuwa mshtaki (tapeli) apewe “haki” yake and akaruhusiwa na koti kubomoa kilichopo kwenye kiwanja. Akabomoa msingi wetu na ukuta na haraka haraka akaanza kujenga ukuta mwingine wa kwake. Hapo ndio tukapata habari kuwa kuna mvamizi wa kiwanja chetu sio kabla ya hapo. Tukasimamisha ujenzi kisheria kwa kuwa mvamizi hakuwa na building permit na pia hakuwa na title deed ambayo ingemwezesha kupata building permit. Title deed tunayo sisi.

Walichofanya makosa ni kuwa katika hati miliki jina la mwenye kiwanja sio mdogo wangu! Sasa inakuwaje anashtakiwa mtu ambaye sio mwenye title deed halafu bila kuhakiki records zilizoko Ardhi ambazo zinaonyesha mwenye kiwanja halisi? Hapo ndio sielewe Judicial system yetu inavyofanya kazi. Huyo hakimu atakuwa naye amevuta senti kidogo?

Nilipokwenda mahakama ya Ardhi Kinondoni nilipewa faili la kesi nzima na niliyoona humo ni mjumuisho wa maajabu ya Musa na Firauni! Documents zote zilitotumika zilikuwa forged kutumia signature ya mdogo wangu. Sijui waliipata wapi. Mdogo wangu anadaiwa alikuwepo kortini kujibu kesi according to the court records. Aliyekuwepo (kama kweli kulikuwa na mtu) hakuwa yeye ni mtu mwingine ambae bilsa shaka amepandikizwa.

Sasa nimeamua kula nao sahani moja hawa wavamizi tuone mwisho utakuwa nini. Nasikia wako ruthless na wana uwezo wa kutumia magazeti na maripota walioko kwenye payroll yao. Nimeambiwa wana pesa nyingi sana na uwezo wa kuwanunua mahakimu, polisi, municipal na serikali ya mtaa ili ku support stori yao huko kotini.

Naomba ushauri kutoka kwenu hasa wale wenye uzoefu wa kesi kama hizi za uvamizi wa viwanja: Ili tuwakomeshe mafisadi kama hawa niiendesheje kesi yangu hasa ukizingatia kuwa wana resources kibao!  Nasikia huu ni mchezo wao. Ni kawaida yao kuwaliza watu wasio na nguvu kipesa za kuwashtaki ili wapate haki zao!

Bongo ninayoijua mimi imeingia sumu kama majambazi wanaweza kuwa “so blatant” na kupora viwanja hata vyenye title deed. Tutakimbilia wapi?

Rama
Safarini Dar-es-Salaam
Habari hii imetoka Tanzanet kwa idhini ya Rama (www.tanzanet.org)
  

6 comments:

Anonymous said...

Rama,
Pole sana na yaliyokukuta

Anonymous said...

HAYO MAMBO NI HAKIMU ASIEKUWA NA BUSARA KWANI NA YEYE VILEVILE KAPEWA PESA NA HAO JAMAA YAANI MJAMAA TANZANIA INATISHA KWANI HAO JAMAA WANAKULA NA KILA MKUBWA ALIEKUWA NA MAMLAKA YA KUSAINI KARATASI KAMA KUNA PESA YEYE ANAWAACHIA MATATIZO WATAJIJU HUKO MBELE Y A SAFARI KWA HIO UTAPELI NAO NI BAHATI NASIBU, HUENDA WATAFANIKIWA HUENDA LAA INATEGEMEA NA MTU WANAESHINDANA NAE UKIWA SLAKI UTASHINDWA. WEWE NENDA KAUONE MAMA TIBAIJUKA, AU WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATAKUSAIDIA WENGI WAMESAIDIWA NA WAKUBWA HAO

Mvunja nchi ni mwananchi said...

Rama..

Fanya chini juu, ua chinja...mwone Mama Tibaijuka au Waziri Mkuu Pinda..

Nchi inaoza taratibu tunaiona. Inanuka. Mwalimu Nyerere alisema haya mwaka 1995.

Anonymous said...

Kaka Rama,

pole sana kwa mkasa huo.

Kwa ushauri wangu, anza kwa maafisa ardhi wa wilaya ambapo kiwanja chako kipo, ongea nao na uwaeleweshe, tena bila jazba wala kuonyesha kukasirishwa sana. Usijaribu kujionyesha unatoka majuu, watajua unazo.

Then jaribu kufuatilia wizarani pia kwa maafisa wanaoshughulikia ardhi.
Usiende kwa wakubwa, hawa wa chini watafanya kila jitihada wakukwamishe.

Mchezo wote kwa sakata kama hili mara nyingi unafanywa na maafisa wa
ardhi, wilayani na wizarani.

Anonymous said...

Ukitaka kwenda na hii kesi kisiasa kwa kuenda ofisi za wilaya nk hutopata chochote, kwasababu hii kesi imehukumiwa mahakamani inabidi utafute wakili mzuri na ukate rufaa pia utafute ushahidi ili afungliwe mashtaka ya kugushi. Kitu ambacho utakifuata ofisi ya wilaya ni nyaraka za kusaidia katika ushahidi wako.

Anonymous said...

BRO SIKILIZA WEWE NENDA MOJA KWA MOJA OFISI YA RAIS SEMA NI MTU UMETOKA NORWAY UNAHOJA YA KUONGEA NAE OFFICIAL HUTAKATAZWA UTASUBIRI SIKU 2 MPKA 5 LAKINI UTA MUONA , UKIMUONA ANZA FUNGUA UKURASA , MWAMBIE YEYE KILA SIKU ANAKUJA HUKU ULAYA NA KUTUSHAWISHI KUJENGA NYUMBANI SASA UMEFIKA WAKATI WAKO MBEBA BOX UKO TAYARI NDIO UNAKUTANA NA WASANIII WA NAMNA HIO! SASA INA MAANA WATANZANIA WOTE WALIOKO NJE HII ISSUE WANAYO NA WOTE WANAOGOPA SASA MAMBO YA NYUMBANI, NA FUMO WOTE HUU WA KITAPELI . SASA TWENDE TUKASHITAKI WAPI? HALAFU UNAOMBA NA KUMUONA MAMA TIBAIJUKA KESI YAKO ITASIKILIZWA MNAMO ONE WEEK.

UKILAZA DAMU AU NDIO HUNA MUDA WA KUFATILIA KESI HIO KIKAMILIFU BASI UMEPOTEZA HAKI YAKO HIVI HIVI.

TAKE CARE