Wednesday, April 11, 2012

Ahmed Ben Bella afariki dunia.

Ahmed Ben Bella.

Rais wa kwanza wa Algeria, Ahmed Ben Bella amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Ben Bella amefariki nyumbani kwake mjini Algiers.

Algeria ilipata uhuru wake toka kwa Wafaransa mwaka 1962 na tarehe 15 Septemba 1963, Ahmed Ben Bella akawa Rais wa kwanza wa nchi hiyo hadi tarehe 19 Juni 1965 alipopinduliwa na waziri wake wa ulinzi, Bw. Houari Boumédienne.

Baada ya kupinduliwa, Ben Bella aliwekwa jela na baadae kwenye ulinzi nyumbani kwa miaka 24.

No comments: