Saturday, April 07, 2012

Steven Kanumba afariki dunia



Mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.


No comments: