Saturday, April 14, 2012

TAFAKARI...! CHUKUA HATUA!!
Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?

 1. Matumizi nyumbani;
 2. Chakula,
 3. Umeme,
 4. Gesi,
 5. Maji,
 6.  Soda/juisi za wageni
 7.  Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu
 8. Matibabu hospitalini,
 9.  pesa ya walinzi kwa mwezi,
 10. sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya,
 11. Zaka ya kanisani na misikitini
 12. Kupanda Mbegu/ Sadaka Shukurani ya Neno
 13. Tozo za flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo)
 14. Madalali wa nyumba/viwanja
 15.  Pango la nyumba
 16.  Fremu ya biashara/ofisi
 17. Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]
 18.  Mafuta ya gari
 19. Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa)
 20. Tozo za kuegesha magari
 21. Makato ya Mikopo
 22.   Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf
 23.  Rambirambi ya mfiwa mtaani au ndugu
 24. Michango ya harusi/send off/kitchen party ya ndugu au rafiki
 25.  Zawadi ya harusi/ sendoff/kitchen party
 26. zawadi ya kumuaga mfanyakazi mwenzenu
 27. zawadi michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara na birthday
 28. Michango ya birthday party na zawadi ndugu wa kule kijijini
 29. Mshahara wa Hausigeli na na hausiboi
 30.  Bodaboda,
 31. teksi na bajaj
 32.  Duka la dawa
 33.  Tuisheni ya mtoto
 34.  Kuchangia wahanga wa mabomu, mafuriko na vistula.
 35.  Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa,
 36.  Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu
 37. Chakula cha mbwa
 38. Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa
 39.  Kuchangia Uinjilisti Masasi /DRC
 40. Auting ya kitimoto
 41.  Ujenzi wa Nyumba Mwabepande
 42.  Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa)
 43. Kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi
 44. Maji ya Traffik
 45.  Chai ya Nesi na Daktari,
 46. Kahawa ya Hakimu, Karani na PP
 47. Vishoka waunganisha maji na umeme
 48. Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa
 49. Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba,
 50. kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.
 51.  umeme na gesi vilivyopanda bei,
 52. maji yaliyoadimika,
 53. bado contingency maana huu usafiri unaotembelea ball joint,bush,fen belt havijafa...bado service,
 54. bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei na restaurants  
 55. sare,baby show...
 56. bado hujatoa watoto outing jumapili n.k
 57. Kutunza wazazi/Wakwe
 58. Kuchangia ujenzi wa barabara/zahanati nyumbani utokako na mjini uishipo nk....nk


Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "...Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaaa..."

Ukifikiria kwa makini unajiuliza watanzania wanasurvive vipi kwa style hii??? 

Imeletwa kwenye blogu toka Tanzanet (www.tanzanet.org)

No comments: