Saturday, May 26, 2012



NIDA yafichua mbinu za matapeli


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, amesisitiza kuwa fomu kwa ajili ya kupatiwa vitambulishio vya taifa haziuzwi na wanaofanya hivyo waripotiwe ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Kwa mujibu wa Maimu,  vitendo hivyo vinalenga kuwahadaa wananchi. Amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuwafichua wanaojihusisha na uuzaji huo wa fomu hizo, ambao ni kinyume cha taratibu, kanuni na sheria ya usajili.
“Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), haijaanza kutoa fomu zozote za usajili kwa wananchi wa mikoani, zaidi ya mazoezi ya usajili kwa watumishi wa umma kwa Dar es Salaam na Zanzibar na zoezi la majaribio Wilaya ya Kilombero, Morogoro lililofanyika  Machi, mwaka huu. Usajili rasmi wa wananchi kwa jumla unakusudiwa kuanza mapema Juni mwaka huu, kwa kuanzia na Mkoa wa Dar es Salaam.”
Kutoka Tanzania Daima

No comments: