Tuesday, June 12, 2012

Dar es Salaam

Kuagwa kwa muasisi wa CHADEMA, marehemu Mohammed “Bob” Makani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi wa Chama hicho Bob Makani.Picha zote na Freddy Maro-IKULU

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Salma Kikwete waliungana na viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho.

No comments: