Saturday, June 16, 2012Kuhusu Utanganyika: Shetani Unayemjua ni Bora Kuliko Malaika Usiyemjua


Wakuu,

Watanzania wengi wamezaliwa baada ya Aprili 26, 1964 kwa hiyo hawaijui Tanganyika, wanasoma tu kwenye makabrasha. Kama hiyo si sahihi sasa basi Watanganyika walioishi Tanganyika huru iliyodumu kwa miaka takriban 4 (1961-1964) wanaijua vizuri Tanzania kuliko Tanganyika iliyodumu muda mfupi! Wanaoidai Tanganyika hawajui kwamba kuna Tanganyika za aina kadhaa:

1. Tanganyika ya kabla ya Mjerumani ambayo haikuwa na mipaka (Pre-1884),
2. Tanganyika ya Mjerumani ambayo ilikuwa na mipaka iliyojumuisha Rwanda na Burundi (1884-1919),
3. Tanganyika ya Mwingereza ambayo haijumuishi Rwanda na Burundi (1919-1961),
4. Tanganyika ya Nyerere ambayo ilidumu kwa muda mfupi (1961-1964),

Kwa hiyo wanaoipigania "Tanganyika" ni ipi hasa na kwa nini? Hiyo Tanganyika mpya ina siri gani ambayo itatukwamua kwenye lindi la umaskini? Sio tukiipata hiyo "Tanganyika mpya" tutakuta ufisadi bado unatutafuna kisawasawa kama kawaida? Hivi Watanzania tumekosa kabisa viongozi wa kutusaidia kujua matatizo ya kweli ya nchi yetu na kuyamaliza "once and for all" badala ya kutuletea "mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya" huku tukiacha matatizo halisi ya ufisadi, wizi, mikataba mibovu, ahadi hewa, udini, kututafuna?

Si afadhali kuendelea na shetani tunayemfahamu (Tanzania) kuliko kung'ang'ania malaika (Tanganyika) tusiyemfahamu? Maana tumeonjeshwa na WANAUAMSHO kwamba tatizo ni nyumba za Ibada, si Muungano!

Tukiwasikiliza hawa jamaa tutacheza ngoma tusyoijua, tutahenyeshwa kisawasawa kama Wakenya wanavyohenyeshwa na Al-Shabaab! Mambo haya yaluanza kama mchezo kama yanavyoendelea kwenye Utawala wa JK na bahati mbaya kuna mkono wa Serikali kwenye vuguvugu ya Uamsho! Sasa hivi wamehamia kwa Dr Ndalichako, Sensa, nk. Kesho utasikia mengine mengi! Tuiache Tanzania yetu kama ilivyo, tuweke kipaumbele kwenye "matatizo halisi"


Nawasilisha!!!

Kutoka kwa mdau anajiita Lord Justice

No comments: