Sunday, June 10, 2012


Muasisi wa CHADEMA afariki dunia

Mohammed "Bob" Makani.

Kwa taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa aliyekuwa Muasisi wa CHADEMA, Mohammed "Bob" Makani amefariki Dunia jana jioni jijini Dar kwenye hospital ya Aghakhan, Mwenyekiti wa CHADEMA amethibitisha hilo kwa njia ya simu kutoka Kanda ya kusini walikokuwa wakifanya mikutano yao ya hadhara.

Mh Mbowe amesema kuwa Marehemu Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi, amesema kuwa Mwili wa Marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi.
  Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.


No comments: