Tuesday, June 26, 2012

Mwanamama alazimika kukaa na maiti ndani ya Kenya Airways


Mwanamke raia wa Sweden alilazimika kukaa na maiti kwa zaidi ya saa kumi, New York Daily limeeleza.

Lena Patterson ripota wa ‘Radio Sweden’ alitanabaisha kuwa abiria mwenzake aliyekadiriwa kuwa na miaka thelathini hivi alionekana mgonjwa wakati aliopopanda katika ndege hiyo iliposimama katika uwanja wa ndege wa Schiphol, Amsterdam.

“Alionekana mwenye kutokwa jasho, wahudumu wa ndege walikuwepo lakini hawakujali na ndege iliondoka”

Abiria huyo alifariki baadaye usiku pamoja na jitihada za wahudumu na abiria kujaribu kumsaidia.

Patterson aliyekuwa akielekea Tanzania kwa mapumziko alilazimika kukaa na maiti huyo mpaka mwisho wa safari.

“Niliomba kuhama lakini walisema hakukuwa na nafasi nyingine”  Alisema. Anasema aliporudi nyumbani kwake aliwaandikia barua pepe uongozi wa KQ na walikubali kumrudishia nusu ya kiasi alicholipa ambacho ni kama dola 1,400 kwa tiketi.

Abiria huyo ameridhika na kiasi hicho.

No comments: