Friday, June 29, 2012

Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara, amenusurika kifo


Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara, amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea leo Igunga mkoani Tabora wakati akiwa safarini kuelekea Mwanza akitokea Dodoma.

Gari la Waziri Dk. Mukangara linadaiwa kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulipita roli la mizigo na kutaka kugongana uso kwa uso na basi la Green Sta lililokuwa likitokea Mwanza.

Waziri, Msaidizi wake na dereva walipata majeraha na kutibiwa katika Hospitali ya Nzega Mkoani Tabora.

No comments: