Saturday, July 21, 2012Mbunge wa Misri ajifedhehesha


Mbunge wa Misri wa chama cha Kiislamu chenye msimamo mkali, amekutikana na makosa ya kuvunja adabu ya kijamii, kuhusu tukio ambapo amekutikana anafanya mapenzi ndani ya gari lake.

Kesi hiyo imewatia aibu Waislamu wanaoitwa Salafi - ambao wanadai kuwa wanaume watengwe kabisa na wanawake.

Mbunge huyo, Ali Wanis, alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na nusu, kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi, na kwa kumshambulia askari polisi.

Mbunge huyo ni wa chama cha Nour, kwenye bunge la mwanzo kuundwa baada ya utawala wa Rais Mubarak - bunge ambalo lilifutwa mwezi uliopita baada ya mahakama kuamua kuwa bunge hilo siyo halali.

Chanzo: BBC Kiswahili

No comments: