Tuesday, July 24, 2012

Rais wa Ghana John Attah Mills afariki


Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata matibabu.

Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.

Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo. Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais. Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.

"Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.

Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali. Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.

Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.

Mills, anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.

Chanzo: BBC Kiswahili

No comments: