Monday, July 16, 2012

Usajili wa magari kwa kutumia majina waanza TRA
Kuanzia mwaka mpya wa fedha (2012-2013) Mamlaka ya Mapato Tanzania imeanza kusajili magari kwa kutumia majina ikiwa ni nyongeza ya kutumia namba kama ilivyokuwa imezoeleka na wengi. Pichani juu na chini ni gari la kwanza kupewa usajili huo wa kutumia jina.

Usajili huu wa kutumia jina unaweza kufanyika kwenye ofisi yoyote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayohusika na usajili wa magari katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Chanzo: wotepamoja.com

No comments: