Tuesday, August 07, 2012


Jumuia ya Watanzania; Norway, Sweden, Finland na Denmark


YAH:  HIFADHI YA JAMII KWA DIASPORA (WESTADI).

Kwa Jumuia ya Watanzania,

Ubalozi  wa Tanzania, Sweden, umepokea barua kutoka Wizara yetu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikitufahamisha kuhusu kuanzishwa kwa huduma ya HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA WAISHIO NJE – Welfare Scheme for Tanzanians in the Diaspora (WESTADI).

Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) sasa imepanua huduma zake kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora). Lengo la bima hii ni kuondoa adha kubwa inayoipata Diaspora kuhudumia ndugu wanapougua Tanzania, au diaspora anpougua akiwa likizo Tanzania na Mtanzania anapofariki akiwa nje ya nchi.

Chini ya WESTADI, mwanachana atatakiwa kulipa ada ya dola za Kimarekani mia tatu (USD 300) kwa mwaka ili kupata mafao kama ifuatavyo;

1.   Huduma va matibabu kwa wategemezi wanne (4) wa Mwanachana ambao wanaishi nyumbani (Tanzania);
2.   Huduma ya matibabu kwa Mwanachama pindi atakaposafiri kuja Tanzania wakati wa likizo au kwa sababu zozote zile;
3.   Huduma za kusafirisha mwili wa Mwanachama kuja nyumbani iwapo atafariki akiwa nje ya nchi pamoja na kulipia tiketi ya msindikizaji mmoja.
4.   Hudurna ya mazishi katika nchi anayoishi Mwanacharna ikiwa amechagua kuzikwa nchi aliyopo. 

Mtegemezi atachagua hospitali iliyo ndani ya mkoa husika na huduma kwake zitaanza mara moja baada ya kuthibitishwa kwa ingizo la pesa za Bima ya Mtu aliyeko nje.

Huduma zitasimama mara punde mwenye bima atakapositisha na kuondoa michango ya pesa za kila mwaka.

Ili kufahamu zaidi juu ya suala hili tafadhali rejea taarifa ya uzinduzi wa WESTADI uliofanyika Septemba 2011 wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Watanzania waishio, Dikota, Marekani bofya (HAPA).  Mgeni wa heshima katika uzinduzi huu alikuwa Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Maelezo zaidi juu ya Mfuko huu na namna ya kuwa mwanachama yako katika tovuli ya NSSF (http://www.nssf.or.tz).

Pia kwa taarifa ya mfano kuonyesha faida ya mfuko huo kwa wanachama wake bofya hapa. (HAPA)

Ubalozi unaomba muisambaze taarifa hii kwa jumuia ya watanzania na muwasihi wawafahamishe na wengine. 

UBALOZI WA TANZANIA,
Näsby Allé 6
183 55 Täby

Simu: +46 8 732 24 30/31
Fax: +46 8 732 24 32
Baruapepe: mailbox@tanemb.se
SWEDEN

No comments: