Thursday, August 02, 2012


Nipo tayari kunyang´anywa kadi – Hassan Nassor Moyo


MUASISI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Hassan Nassor Moyo amesema yuko tayari kurejesha kadi ya chama chake iwapo atalazimika kufanya hivyo huku akisisitiza kuunga mkono Muungano wa Mkataba.Mwanasiasa Mkongwe Hassan Nassor Moyo Akionyesha hati za makubaliano ya mambo ya Muungano mbele ya Waandishi wa Habari mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wake hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Rumaisa Bwawani Zanzibar.

Mwandishi wa Habari Mwandamizi Salim Said Salim akimkaribisha Mwanasiasa Mkongwe Hassana Nassor Moyo kuzungumza na Waandishi mbalimbali kuhusiana na Mambo ya Muungano hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Rumaisa Bwawani Zanzibar.


Baadhi ya Waandishi wa Habari mbalimbali waliohudhuria Katika Mkutano wa Mwanasisa Mkongwe Hassan Nassor Moyo akizungumzia mambo ya Muungano hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Rumaisa Bwawani Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai, Maelezo-Zanzibar


No comments: