Tuesday, September 04, 2012

Njia Ninayopendekeza Ya Kumsaidia Mjane Wa Marehemu Daudi Mwangosi.....


Maggid Mjengwa http://www.mjengwablog.com/ 


Ndugu zangu, 


Kuna wenzetu kadhaa walioniandikia kutaka niandae utaratibu wa kukusanya michango ili imfikie mjane wa Marehemu Daud Mwangosi ambaye sasa anakabiliwa na jukumu kubwa la kuwalea watoto wanne baada ya kuondokewa na mumewe.
                          
Ninachopendekeza;

Kwa vile ni ukweli ambao hata mimi nilipokuwa msibani jana niliusikia; changamoto ya mjane wa marehemu kutunza watoto. Nadhani njia nzuri ya kumsaidi mjane huyu wa marehemu ni kwenye suala la elimu ya watoto wake wanne ambaye wa mwisho ana miama miwili tu.

Yakufanya:
1. Tusubiri kwanza mjane arudi Iringa kutoka kumzika mumewe huko Tukuyu.
2. Mimi nitakwenda kwa mjane na kumwelezea dhamira ya baadhi yenu humu kijijini Mjengwablog kutaka kumsaidia japo kwa kuchangia elimu ya watoto wake.
3. Aniambie ni watoto wake wangapi walio shuleni na kiasi gani kinahitajika kwa ada ya muhula au mwaka.
4. Wenye kujisikia kumchangia wafanye hivyo kwa kupitia akaunti yake ikiwamo M- Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kama anazo zote. Vile vile kwa Western Union.
5. Michango hiyo itumwe moja kwa moja kwake na yeye atunze kumbukumbu ya waliomchangia na anijulishe pale kiasi kinachohitajika kama kimepatikana au la. Nami nitawajulisha juu ya hilo kupitia hapa.

Ni hayo tu, nakaribisha michango yenu ya maoni.
Mwenyekiti Wenu,

Maggid Mjengwa,
Iringa.
+255 788 111 765

No comments: