Sunday, October 28, 2012

Tumeanza majira ya theluji (Winter)


Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 28 Oktoba 2012, hapa Norway (Skandinavia) tumebadili majira na kuingia majira ya theluji (Winter time). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tumerudisha saa moja nyuma. 

Tuna tofauti ya masaa mawili na saa za Afrika Mashariki kwenye majira ya theluji. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 4 za asubuhi,
Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summer). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.


Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Winter). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.

No comments: