Na
Haruni Sanchawa
MWANAMKE mmoja, Esther Meshaki amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Januari 18, 2012 hadi leo na hajawahi kutembelewa na ndugu yake au rafiki yeyote, Uwazi limegundua.
Afisa Habari
wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema wiki iliyopita kuwa
mgonjwa huyo aliletwa na polisi waliodai kumuokota barabarani katika eneo la
Temeke akiwa hajitambui.
“Wataalamu
wetu wamejitahidi kutoa huduma kwa mgonjwa huyu kufikia kiwango cha kuweza
kuongea mwenyewe na kujitambua vizuri.
“ Changamoto
tuliyonayo ni kuwa mgonjwa huyu tangu alazwe hakuna ndugu wala jamaa yake
yeyote aliyejitokeza. Hivyo kwa sasa tunatafuta ndugu wa mgonjwa huyu ambaye
amepata nafuu ili aweze kujiunga na familia yake,” alisema Aligaesha.
Alifafanua
kuwa katika kufanya udadisi imegundulika kuwa Esther alizaliwa Kigoma vijijini
katika Kijiji cha Kigogwe mwaka 1985. Kabila lake ni Muha na anasema mama yake
anaitwa Dotto Alfred na baba yake anaitwa Meshaki Alfred ambao hata hivyo,
walitengana.
“Ndugu,
jamaa au yeyote mwenye taarifa za mgonjwa huyu naomba awasiliane na Ofisi ya
Uhusiano Hospitali ya Muhimbili kupitia namba 0755 648 636,” alisema afisa
habari huyo.
No comments:
Post a Comment