Wednesday, March 13, 2013

MZEE KINGUNGE ATAKA VIONGOZI KUENZI LUGHA YA KISWAHILI


Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati  uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi  katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na kulia ni Brigedia Hashimu Mbita.


Na Frank Shija na Benedict Liwenga - Maelezo

VIONGOZI wahimizwa MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwataka viongozi nchini kukienzi na kuthamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mzee Kingunge ambaye alikuwa  mgeni ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee,  jijini Dar es Salaam .

“Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.

Aidha  Mzee Kingunge anawaasa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali mfano Bungeni.

Hata hivyo, aliunga mkono  lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.

Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata  alama 90 hadi 95,lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.

“Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimu ya Chuo Kikuu,”alisema. Huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.

Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo  Profesa Mugyabuso Mulokozi na  Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi   fasihi za Watanzania.

No comments: